NEWS

Tuesday, 25 January 2022

Mbunge Ghati aipa Hospitali ya Wilaya Butiama msaada wa mashuka



MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete ameipatia Hospitali ya Wilaya ya Butiama misaada ya mashuka na ndoo za kuhifadhi taka, vyote vyenye thamani ya shilingi milioni mbili.

Amekabidhi misaada hiyo kwa uongozi wa hospitali hiyo leo Januari 25, 2022, ambapo pia amepata fursa ya kuwajulia hali wagonjwa, kuzungumza na watumishi na kufahamu changamoto zao, ili aweze kushirikiana na mbunge wa Butiama kuzitafutia ufumbuzi.


Mbunge Ghati (mwenye miwani mbele) akikabidhi misaada hiyo

Katika ziara hiyo, Mbunge Ghati amefuatana na Mbunge wa Butiama, Jumanne Sagini, viongozi wa CCM, UWT, UVCCM Wilaya ya Butiama na madiwani wa halmashauri ya wilaya hiyo.


Mbunge Ghati (wa tatu kulia mbele) katika picha ya pamoja na viongozi aliofuatana nao katika ziara hiyo. Wa tatu kushoto ni Mbunge Sagini.

Mbunge Ghati amesema amewiwa kutoa misaada hiyo ili kuwasaidia wagonjwa wanaolazwa hospitalini hapo.

Mbunge Sagini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, amemshukuru Mbunge Ghati kwa moyo huo wa kujitolea na kumwahidi ushirikiano zaidi katika masuala ya maendeleo ya wananchi.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages