NEWS

Wednesday 9 February 2022

GSN atangaza neema kwa vijana Rorya
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Gerald Samwel Ng’ong’a (pichani juu) ametangaza kuanzisha kituo cha kutoa mafunzo ya kozi mbalimbali za ufundi kwa vijana waliohitimu kidato cha nne katika halmashauri hiyo.

Kwa mujibu wa Ng’ong’a ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Rabour kupitia chama tawala - CCM, mpango huo unalenga kusaidia mamia ya vijana ambao hawakufanikiwa kuendelea na masomo ya kidato cha tano baada ya kuhitimu kidato cha nne kwa miaka ya hivi karibuni.

“Nitapita kila tarafa kuzungumza na vijana waliofeli mtihani wa kuhitimu kidato cha nne, ili tuzungumze namna ya kuwasaidia kulingana na mahitaji yao. Kufeli mtihani sio mwisho wa maisha,” Ng’ong’a maarufu kwa jina la GSN, ameiambia Mara Online News ofisini kwake, juzi.

Ametolea mfano mafunzo ya ufundi bomba ambayo amesema yanaweza kusaidia vijana wengi kutokana na fursa za utekelezaji wa miradi mikubwa ya maji kupitia wizara ya maji.

“Mafunzo ya ufundi yatatengeneza ajira ili miradi - mfano ya maji inayotekelezwa Rorya inakuwa na fursa kama vijana watakuwa na utaalamu, ili mwisho wa siku tukutane na vijana hao katika sekta ya maendeleo,” Ng’ong’a.

Wizara ya maji inapanga kutekeleza mradi mkubwa wa maji utakaowezesha wananchi wa wilaya za Rorya na Tarime kupata huduma ya maji safi ya bomba kutoka Ziwa Victoria.

Mbali na ufundi bomba, Ng’ong’a amesema kituo hicho kitatoa mafunzo ya kozi ya ushonaji, miongoni mwa nyingine.

(Habari na picha: Mara Online News)

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages