NEWS

Friday, 4 March 2022

Kumekucha Siku ya Wanawake Duniani na Utalii wa Ndani Serengeti



KUNDI kubwa la watalii wa ndani (baadhi yao pichani juu) kutoka maeneo mbalimbali mkoani Mara, limewasili katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Lamai mapema leo asubuhi, ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani, ambayo kilele chake kitaadhimishwa kimkoa wilayani Butiama, Machi 8, mwaka huu.


Meneja Miradi wa ATFGM Masanga, Valerian Mgani (wa pili kulia) katika picha ya pamoja na watalii wa ndani wenzake ndani ya Hifadhi ya Serengeti, leo asubuhi.


Sehemu ya kundi la watalii wa ndani waliowasili Hifadhi ya Serengeti, leo asubuhi.
Makundi ya nyumbu ni miongoni mwa vivutio vikubwa vinavyoipamba Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Aidha, kuelekea maadhimisho hayo, kundi kubwa la wanawake kutoka Tarime, Rorya na Mugumu linatarajiwa kutembelea hifadhi hiyo Jumapili ya Machi 6, mwaka huu.

“Maandalizi ya safari hiyo ya Jumapili yamekamilika na wageni wa kundi hilo watapitia lango la Ikoma,” amesema Jacob Mugini, Mkurugenzi wa Mara Online Safaris - kampuni inayoshirikiana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuhamasisha utalii wa ndani.


Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mara, Neema Ibamba (kushoto) katika picha ya pamoja na mtalii wa ndani mwenzake ndani ya Hifadhi ya Serengeti, leo asubuhi.

Kampuni ya Mara Online Safaris inahamasisha utalii wa ndani Serengeti kupitia vyombo vya habari vya blogu hii ya Mara Online News na gazeti la Sauti ya Mara.


Wanawake mkoani Mara wameendelea kuhamasika kushiriki safari ya kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kuelekea Siku ya Wanawake Duniani ambayo huadhimishwa Machi 8 kila mwaka. Kulia ni mmoja wa wanawake hao aliyefika ofisi za Mara Online juzi kununua tiketi yake tayari kwa safari hiyo itakayofanyika Machi 6, 2022.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages