NEWS

Wednesday, 9 March 2022

Madiwani Tarime Vijijini wapiga jeki ujenzi wa shule mpya


Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) Simon Kiles jana ameongoza madiwani wa halmashauri hiyo kuchangia mifuko ya saruji 26 katika mradi wa ujenzi wa shule ya msingi mpya ya Nyabinembu iliyo katika kata ya Nyakonga.

“Ujenzi wa shule hii mpya ya Nyabinembu utapunguza adha ya kusafiri umbali mrefu kwa wanafunzi kufata huduma ya elimu shule ya msingi Kebweye. Pia nitasimamia ujenzi wa boma la darasa mpaka kukamilika”, alisema Kiles .



No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages