NEWS

Thursday 10 March 2022

Hali si shwari mto Mara, samaki waangamia, harufu ya maji yatisha


KUNA hali ya sintofahamu inayohusisha kufa kwa samaki aina ya sato na kusababisha harufu kali ya uvundo katika baadhi ya maeneo ya mto Mara.

Maeneo ya mto huo yaliyoripotiwa kuathirika hadi sasa yako katika baadhi ya vijiji vya wilaya ya Rorya mkoni Mara, Tnzania.

“Samaki wanakufa na kuna harufi. Tumechukua sampuli kujua chanzo nini,” amesema ofisa mwandamizi wa Serikali aliye kwenye timu maalum iliyotumwa katika vijiji hivyo.

Kwa mujibu wa ofisa huyo, timu hiyo inahusisha wataalumu katoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB), Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Mkuu wa Wilaya ya Rorya.

“Tunaelekea sasa hivi katika vijiji ambavyo samaki wamekufa,” ofisa huyo ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu leo.

Baadhi ya vijiji hivyo ni Kwibuse, Nyanchabakenye na Mara-Sibora, kwa mujibu wa vyanzo vyetu vya habari.

Uchimbaji wa madini unatajwa kuwa moja ya tishio la uhai wa mto huo ambao ni muhimu kwa ustawi wa maisha ya maefu ya wananchi na ikolojia ya Serengeti.

Mto Mara ni mto wa kimataifa unaoanzia kwenye chemichemi za Enopuyapui katika misitu ya Mau nchini Kenya na kupita katika mbuga ya Masai Mara, Kenya, Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kabla ya kutiririsha maji ndani ya Ziwa Victoria upande wa Tanzania.

Hata hivyo, mto huo unaripotiwa kuwa na matishio mbalimbali, ikiwemo uchambaji wa wa madini.

Mbali na uhifadhi wa wa ikolojia ya Serengeti - Mara, Bonde la Mto Mara lina mchango mkubwa katika ustawi wa maisha ya watu zaidi ya milioni 1.1 katika nchi za Tanzania na Kenya.

Mto Mara una urefu wa kilomita za mraba 13,504, kati ya hizo, asilimia 65 ziko Kenya na asilimia 35 Tanzania.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages