NEWS

Wednesday 9 March 2022

Malkia akaunti yawawezesha wanawake kumiliki viwanja


Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakitoa huduma kwa wateja wilayani Butiama

WANAWAKE mkoani Mara wamesema utunzaji wa akiba kupitia akaunti ya malkia kupitia benki ya CRDB imewawezesha kuweza kumiliki viwanja.

Wakizungumza na Waandishi wa Habari katika maadhimisho ya siku ya wanawake yaliyofanyika kimkoa wilayani Butiama,wamesema kujiwekea akiba ni mwanzo wa mafanikio.

Wamesema kabla ya kufungua akaunti hiyo walipata elimu kutoka benki ya CRDB tawi la Musoma juu ya umuhimu wa Malkia akaunti na kuamua kufungua.

Mmoja wa wanawake hao aliyejitambulisha kwa jina la Mariamu Juma,amesema ameweza kumiliki kiwanja na kupata hati ya kumiliki kutokana na kuweka akiba kupitia Malkia akaunti..

Mariam amesema mwanamke mpambanaji anaweza kumiliki kiwanja na mali iwapo atakuwa na malengo ya kuweza kufanya jambo.

Amesema benki ya CRDB kupitia akaunti ya Malkia inayo malengo mazuri kwa mwanamke katika kumuwezesha kupitia akiba anayoiweka kwaajili ya baadae.

' Naishukuru benki ya CRDB kwanza kwa elimu ya ujasiliamali niliyoipata Musoma na baadae kufungua akaunti ya Malkia.

' Akiba niliyoiweka kupitia akaunti hii imeniwezesha kumiliki kiwanja na kupitia maadhimisho ya siku ya wanawake nimeweza kukabidhiwa hati ya kumiliku",amesema Mariam.

Kwa upande wao watumishi kutoka benki ya CRDB walioshiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani wilayani Butiama wamesema bado fursa ipo kwa wanawake kuweza kujiunga na akaunti ya Malkia kwa kuwa inamanufaa makubwa.

(Na Shomari Binda-Butiama)
No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages