MVUA iliyoambatana na upepo mkali imeezua na kubomoa nyumba zaidi ya 20 katika kijiji cha Nyakunguru wilayani Tarime, Mara.
Tukio hilo limetokea juzi jioni katika kitongoji cha Nyamuma, kwa mujibu wa Ofisa Mtendajii wa Kijiji hicho, Zakayo Chacha Wangwe.
“Mvua ilikuwa na upepo mkali na nyumba 16 zilizoezuliwa ni za kawaida na tano ni za kudumu [zilizojengwa kwa matofali],” Wangwe ameiambia Mara Online News leo mchana.
Amesema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
Nyakungu ni kimojawapo cha vijiji vilivyo jirani na Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.
“Tayari tumetoa taarifa kwenye mamlaka za juu na wananchi wamewasaidia [wamewapa hifadhi] waliopatwa na mkasa huu,” amesema Wangwe.
(Imeandikwa na kuhaririwa na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment