NEWS

Sunday 17 April 2022

Ng’ong’a ashiriki ibada ya Pasaka Kanisa Katoliki Buturi na kuchangia ujenzi wake, ahamasisha sensa ya watu na makaziMWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Gerald Ng’ong'a (pichani juu), mapema leo ameungana na waumini wengine kushiriki ibada ya Pasaka katika Kanisa Katoliki - Kigango cha Buturi.

Ng’onga ambaye kwa upande mwingine ni Diwani wa Kata ya Rabuor, ametumia nafasi hiyo pia kutoa msaada wa shilingi 200,000 kuchangia gharama za umaliziaji wa ujenzi wa kanisa hilo.


Ng'ong'a (katikati) akiteta jambo na viongozi wa kanisa hilo, miongoni mwa waumini wengine.

Aidha, Ng'ong'a amewatakia wananchi wa wilaya ya Rorya Pasaka njema na kuisherehekea sikukuu hiyo kwa amani na upendo.

Katika hatua nyingine, Mwenyekiti huyo wa halmashauri ametoa wito wa kuhamasisha wananchi wa wilaya hiyo kuwa tayari kujitokeza na kutoa ushirikiano wa kutosha katika shughuli ya Sensa ya Watu na Makazi.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages