NEWS

Tuesday 5 April 2022

Radi yajeruhi wanawake wawili TarimeWATU wawili wamejeruhiwa kwa radi katika kijiji cha Kerende, wilaya ya Tarime mkoani Mara.

“Wote waliojeruhiwa ni wanawake wawili na wamekimbizwa katika kituo cha afya Nyamongo,” Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Kerende, Muniko Magabe ameimbia Mara Online News kwa njia ya simu muda mfupi baada ya tukio hilo, jana jioni.

Magabe amefafanua kuwa waliojeruhiwa ni wakazi wa kitongoji cha Mogosi na kwamba tukio hilo lilitokea saa 12:30 jioni.

“Mmoja amejeruhiwa mguu na mwingine amejuruhiwa tumbo,” amesema mwenyekiti huyo bila kuwataja majina.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages