NEWS

Tuesday 5 April 2022

Ripoti ya uchafuzi Mto Mara yatua BungeniWABUNGE wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania leo wanapokea ripoti ya matokeo ya uchunguzi wa uchafuzi wa maji uliosababisa vifo vya samaki na harufu mbaya katika Mto Mara.

Spika wa Bunge, Dkt Tulia Ackson amewambia wabunge kuwa ripoti hiyo itawasilisha mbele wabunge ili waweze kufahamu matokeo yake kwa kina.

“Waziri Jafo atakuwapo na wataalmu wake. Lengo letu ni kwamba mpate uelewa kuhusu majibu ya watalaamu wetu,” Spika wa Bunge amewambia wabunge jijini Dodoma leo asubuhi.

Selemani Jafo ndiye Waziri mwenye dhamana ya mazingita Tanzania.

Hivi karibuni ulitokea uchafuzi wa maji na vifo vya samaki katika Mto Mara eneo la Kirumi darajani mkoani Mara, tukio ambalo lilisababisha taharuki kwa wananchi, hususan wakazi wa vijiji vilivyo jirani na eneo lililokumbwa na tatizo hilo.

Siku chache baadaye, Waziri Jafo aliunda Kamati ya Kitaifa ya Watu 11 kwa ajili ya kuchunguza ili kubaini chanzo cha uchafuzi katika mto huo unaotiririsha maji kwenye Ziwa Victoria.


Sehemu ya Mto Mara iliyokumbwa na uchafuzi huo

Mbali na uhifadhi wa wa ikolojia ya Serengeti - Mara, Bonde la Mto Mara lina mchango mkubwa katika ustawi wa maisha ya watu zaidi ya milioni moja kwenye nchi za Tanzania na Kenya.

Mto Mara una urefu wa kilomita za mraba 13,504, kati ya hizo, asilimia 65 ziko Kenya na asilimia 35 ziko upande wa Tanzania.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages