
Mhariri Mtendaji, Jacob Mugini (katikati) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya (DC) ya Butiama, Mwalimu Moses Kaegele nakala ya toleo la wiki hii la gazeti la Sauti ya Mara katika viwanja vya Makumbusho ya Mwalimu Julius K. Nyerere - Butima leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Makumbusho hiyo, Emmanuel Kiondo.
Tukio hilo limefanyika mara baada ya DC Kaegele na Mkurugenzi Kiondo kufanya mazungumzo na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya kitaifa ya miaka 100 tangu kuzaliwa kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, yatakayofanyika Aprili 13, 2022 katika viwanja vya Mwenge kijijini Butiama.
#MaraOnlineNews-Updates
No comments:
Post a Comment