NEWS

Sunday 10 April 2022

Yajue maeneo manne ya kuvutia ambayo binadamu hawezi kufika ulimwenguni



Katika ulimwengu wa sasa, ni vigumu kufikiria mahali ambapo hatuwezi kufika kabisa, na ambapo hapapigwi picha wala kushirikishwa na kutambulishwa kwenye mitandao ya kijamii.

Lakini pia kuna maeneo ambayo bado hayajaguswa na watalii.

Ingawa maeneo mengi sayari zinakaribisha wageni, kuna baadhi ambazo zimepigwa muhuri kutoka kwa umma.

Mara nyingi kwa sababu za usalama, kisheria au kisayansi, ni marufuku kabisa kuweka mguu maeneo hayo.

Tunakualika ujue pande nne kati ya hizi zilizojitenga na dunia:

1. Lango la mwisho wa dunia "Doomsday Vault"



Hili ndio geti la kuingilia "dunia ya siku za mwisho", World Seed Bank huko Svalbard, Norway.

Kipo katika kisiwa cha mbali kiitwacho Spitsbergen, visiwa vya Svalbard, Norway, mlima ambao huficha mita 120 ndani ya eneo la kusadikika.

Takriban kilomita 1,300 kutoka Ncha ya Kaskazini na mita 130 juu ya usawa wa bahari, kwenye barafu kubwa - safu ya kudumu ya barafu iliyoganda ambayo inazunguka geti - husaidia kuhifadhi mamia ya maelfu ya sampuli za mbegu zilizohifadhiwa ndani.

Ni sehemu bora kwa kazi hii kutokana na ukosefu wa shughuli za seismic.

Hata hivyo, ingawa mbegu zimehifadhiwa kwa usalama iwezekanavyo tangu chumba cha kuhifadhia maji kilipofunguliwa mwaka 2008, hakuna njia ya kibinadamu ya kuthibitisha hili.

Hifadhi hiyo inalindwa sana, inahakikisha kwamba mbegu zilizomo zinaweza kuishi kwa maelfu ya miaka ikiwa kuna ulazima.

Hata hivyo katika miaka ya hivi karibuni, wanasayansi fulani wamepatwa na wasiwasi kuhusu kuongezeka kwa halijoto, jambo ambalo limesababisha barafu kuyeyuka.

Mwaka 2020, watafiti wa ndani waliandika majira ya joto zaidi kwenye Svalbard kwenye rekodi.

"Tuliona kuyeyuka kwa barafu," mwanasayansi Kim Holmen wa Taasisi ya Polar ya Norway aliambia BBC.

Hali hiyo ilianza kufuatiliwa miaka michache iliyopita.

Sehemu hii ni muhimu kwa ajili ya kuhifadhi mbegu, katika tukio la janga kubwa la kimataifa, hifadhi ya mazao ambayo inahakikisha urejesho wa viumbe, na kwamba sisi wanadamu hatukosi chakula.

Kila nchi huhifadhi mbegu zake muhimu kwa ajili ya uzalishaji wake wa chakula, lakini Benki ya Mbegu ya Dunia ya Svalbard ni aina ya wafadhili wa kimataifa.

2. Ilha da Queimada Grande: Kisiwa chenye sumu

Ilha da Queimada Grande, inayojulikana kama Ilha das Cobras (kisiwa cha cobras), ni kisiwa kidogo chenye miamba, mapori, hakuna fukwe na ni vigumu kufikiwa, kinapatikana kilomita 35 kutoka pwani ya São Paulo.

Kisiwa hiki kiligunduliwa mwaka 1532 katika msafara wa enzi za ukoloni wa Martim Afonso de Souza.

Ingawa, historia ya Ilha das Cobras ni ya zamani zaidi.

Iliundwa mwishoni mwa enzi ya mwisho ya barafu, kama miaka 11,000 iliyopita, wakati usawa wa bahari ulipoinuka, kikitenganisha mlima kutoka bara na kugeuka kuwa kisiwa.

Kumekuwa kukivutia kwa takriban karne tano zilizopita kwa muonekano usio wa kawaida: kunakaliwa karibu na nyoka pekee: inakadiriwa kwamba kunaweza kuwa na nyoka mmoja hadi watano kwa kila mita moja ya mraba wa kisiwa.



Ni eneo la pili kwa idadi kubwa wa nyoka kwa kila eneo duniani: lina karibu hakta 45, takriban sawa na ukubwa wa uwanja wa mpira - takwimu ambayo ni ya pili baada ya Kisiwa cha Shedao kilichopo nchini China.

Lakini katika kisiwa cha Brazil, spishi ya nyoka wenye sumu kali ilijitofautisha na ndugu zake wa duniani na kuwa lancehead ya dhahabu (Bothrops insularis), aina ya nyoka waliopatikana kwenye kisiwa cha Queimada Grande.

Huwa ni hatari sana ndege aking'atwa mara moja kunamfanya asiweze kuruka tena.

"Sumu ya nyoka ni hatari zaidi kwa ndege kuliko kwa mamalia," mwanabiolojia Marcelo Ribeiro Duarte kutoka Maabara ya Mkusanyo wa Wanyama ya Taasisi ya Butantan, alieleza BBC Brazil.

"Hiyo inathibitisha uwezo mkubwa wa kubadilika kwa aina ya viumbe."

"Kwa vile wanyama wa kisiwa hicho ni wachache sana, bila mamalia wengine (isipokuwa popo), wanyama wakubwa wa aina hii hula ndege wanaohama," mtafiti aliiambia BBC Brazil na mtaalamu wa wanyama wenye sumu Vidal Haddad Júnior kutoka Kituo cha Tiba cha Botucatu.

"Viumbe wadogo wa majini, kwa mfano."

Serikali ya Brazil ilipiga marufuku mtu yeyote kwenda kisiwa hicho, kama hatua ya tahadhari.

Sheria hii inawaruhusu baadhi ya watafiti, ambao ili kutembelea lazima waambatane na daktari ambao watatakiwa kufuata itifaki kali.

Kwa namna yoyote vile, kisiwa hiki cha mbali cha hekta 43 karibu na pwani ya São Paulo hakionekani kuwa mahali pazuri pa likizo.

3. Lascaux: Pango la Ufaransa ambalo lina sanaa ya thamani



Vijana wanne waliokuwa wakitafuta mbwa aliyekuwa ametoweka kupitia kwenye shimo lililo ardhini waligundua pango hili la ajabu kusini mwa Ufaransa mwaka 1940.

Katika hali ya kushangaza zaidi, mbwa wao aliwaongoza kwenye pango lililofunikwa kwa picha za ukutani zinazoonesha wanyama kama vile farasi na kulungu.

Ilianza miaka 17,000 hivi, ilikuwa mojawapo ya mifano iliyohifadhiwa vizuri zaidi na sanaa ya kabla ya historia iliyowahi kugunduliwa, ikiwa na picha kati ya 600 na 1,000 hivi.

Wakati vijana hao walipokuwa wakigundua shimo hili, Vita ya Pili ya Dunia ilikuwa inaendelea.

Miaka minane baadaye, pango la Lascaux lilifunguliwa kwa umma kwa watu ambao walitaka kuona kazi ya mababu zao wa kale.

Mwaka 1963, ziara za umma zilisitishwa. Ukungu ulikuwa kwenye kuta za pango hilo, na hivyo kutishia kuhifadhiwa kwa mchoro ambao ulikuwa katika hali ya hewa isiyopitisha hewa kabla ya ugunduzi wake.

Takriban miaka 60 baadaye, pango hilo bado halijazuiwa kwa umma, ingawa lilijengwa kwa mfano pembeni kidogo ili kuwapa fursa watalii kuendelea kutembelea.

4. Uluru: "kitovu cha ulimwengu"

Uluru, ambapo hapo zamani ilijulikana kama Ayers Rock, kilikuwa kivutio cha watalii kwa miaka mingi, lakini hivi karibuni iliongezwa kwenye orodha ya maeneo ambayo watu hawawezi kutembelea.

Pia inaitwa "kitovu cha ulimwengu", ni moja ya mawe makubwa zaidi kwenye sayari.

Hapo awali, wageni wangeweza kujaribu kupanda kwa mita 348 hadi kwenye kilele, ingawa hiyo ilimaanisha kustahimili joto kali, huku halijoto ya kiangazi ikielea karibu nyuzi joto 47.

Kupanda mwinuko hadi juu kunaweza pia kusababisha shida. Lakini, kwa muda uzuri wake ukishangaza wengi.



Uluru ni pahala patakatifu kwa wenyeji wa asili ya Anangu ambao ni walinzi wa mlima huo na walitaka wageni kuacha kuupanda kwa kuheshimu mila zao.

Shahuku hiyo iliungwa mkono kwa kauli moja na ombi la Bodi ya Hifadhi ya Kitaifa ya Uluru-Kata Tjuta, ambayo ilifanya uamuzi wa kuwazuia watu kufika Uluru mwaka 2017.

Oktoba 25, 2019 ilikuwa siku ya mwisho watu kuruhusiwa kupanda mlima kabla ya marufuku kuanza kutekelezwa. Foleni ndefu za watalii ziliundwa.



Katika utamaduni wa Anangu, Uluru ni ushahidi kwamba viumbe vilikuja duniani wakati ilikuwa bado haijapata umbo na isiyo na uhai.

Walisafiri kwa njia hiyo, wakiunda viumbe hai vya aina mbalimbali, kuelekea Uluru.

Wageni bado wanaweza kutembelea Hifadhi ya Kitaifa ya Uluru-Kata Tjuta. Lakini mlima mtakatifu hauruhusiwi kuupanda wala kuugusa.

Watalii wengi huzuiwa kuchukua picha kutoka angani.

Baadhi ya ndege zinaruka karibu na Uluru katika Hifadhi ya Kitaifa ya Uluru-Kata Tjuta. Chanzo: BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages