NEWS

Saturday 7 May 2022

Watu watano wakiwemo watoto wahofiwa kufa maji wakivuka mto kwa mtumbwi wilayani RoryaWATU watano wakiwemo watoto wanahofiwa kufa maji baada ya mtumbwi waliokuwa wakitumia kuvuka mto Mori katika wilayani Rorya kupinduka.

Habari zilizotufikia hivi bunde kutoka eneo la tukio zinasema tayari mwili wa mtoto wa kike umepatikana, huku juhudi za kutafuta watu wengine waliokuwa kwenye mtumbwi huo ziekiendelea.

Ajali jiyo imetokea leo saa nne asubuhi katika kijiji cha Kowak.

“Mwili wa mtoto kike umepatikana, bado tunawatafuta wengine. Tunatumia njia za kienyeji kama vile kuogelea,” Ofisa Mtendaji wa Kijiji (VEO) cha Kowak, Charles Mwita ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu jioni hii kutoka eneo la tukio.

Kwa mujibu wa VEO huyo, mtumbwi uliopinduka ulikuwa umebEba watu takriban 10, wakiwemo wanawake na watoto.

Hata hivyo, kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, watu watatu waliokolewa mara tu baada ya mtumbwi huo kupinduka.

“Shida ni kwamba hatuna msaada wowote hata kutoka kwa viongozi, wamebaki ni wananchi wanapambana majini, wanawake hao na watoto walikuwa wanavuka kwenda upade mwingine kwenda kanisani,” amesema shuhuda ambaye ni mkazi wa eneo ambalo ajali imetokea.

Wilaya ya Rorya inadaiwa kuwa na miundombinu isiyo salama kwa usafiri wa majini.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages