Apoo Castro Tindwa akiwa kazini |
Waziri wa TAMISEMI Innocent Bashungwa ambaye yupo katika ziara ya kikazi mkoani Mara amemsimamisha kazi aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime(Vijijini) Apoo Castro Tindwa ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Masasi, Mkoani Mtwara
" Inaonekena aliyekuwa mkurugenzi wa Tarime(Apoo Castro Tindwa) ni sehemu ya ubadhirufu huu( CSR) namsimamisha kazi kuanzia sasa na habari zimfikie huko aliko.", Waziri Bashungwa ametangaza wakati akihutubia mkutano wa hadhara baada ya kukagua mradi wa kituo cha afya katka kijiji cha Genkuru wilayani Tarime leo mchana.
Mara Online News itaendelea kukuletea habari zaidi.
No comments:
Post a Comment