NEWS

Wednesday 6 July 2022

Ngicho avunja ukimya, achukua fomu kuwania Uenyekiti CCM Mkoa wa MaraMWENYEKITI wa CCM Wilaya ya Tarime anayemaliza muda wake, Marwa Daudi Ngicho (pichani juu), amevunja ukimya kwa kujitokeza kuchukua fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Uenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Mara.

Ngicho ambaye anatajwa kuwa kada na kiongozi mwenye msimamo usioyumba ndani ya chama hicho tawala, amechukua fomu hiyo katika ofisi za CCM Mkoa wa Mara mjini Musoma, alasiri ya leo Julai 6, 2022.
Marwa Daudi Ngicho (kushoto) akipokea fomu kutoka kwa ofisa wa Ofisi ya CCM Mkoa wa Mara

Katika kinyang’anyiro cha kuwania Uenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Ngicho atachuana na makada wenzake kadhaa, wakiwemo Chadi Marwa, Nyerere Jackson Mwera, Joshua Mirumbe, Wakili Emmanuel Paul Mng’arwe na Mwenyekiti anayemaliza muda wake, Samwel Kiboye “Namba Tatu” anayetetea nafasi hiyo.

Kwa mujibu wa Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Langael Akyoo, tarehe za uchukuaji wa fomu za kuwania nafasi mabalimbali za uongozi ndani ya chama mkoani Mara, ni Julai 2 hadi 10, mwaka huu.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages