NEWS

Tuesday 5 July 2022

Nico achangamkia nafasi ya Katibu Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya TarimeKADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Nicodemus Keraryo (kushoto pichani juu), amechukua fomu ya kutia nia ya nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi wa chama hicho Wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Akizungumza na Mara Online News, baada ya kuchukua fomu hiyo kwa Katibu wa CCM Wilaya ya Tarime, Valentine Maganga, leo Julai 5, 2022, Keraryo amesema pamoja na majukumu mengine, anayo dhamira ya dhati ya kukisaidia chama hicho tawala katika utoaji taarifa kwa ukamilifu na kuongeza msukumo chanya katika jamii.

“Nafasi ya Katibu wa Siasa na Uenezi ni zaidi ya siasa, inahitaji mtu mwenye uwezo wa kutoa taarifa za chama na kufanya maamuzi ya kisera kwa usahihi na umakini,” amesema Keraryo ambaye mwaka 2020 alitia nia ya ubunge jimbo la Tarime Vijijini.

Nicodemus Keraryo - maarufu kwa jina la Nico, amesisitiza kuwa ajenda yake kuu ni kuongeza ufanisi kwenye utoaji wa taarifa, zikiwemo zinazoelezea juhudi zinazofanywa na chama hicho na Serikali katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kisekta.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages