NEWS

Monday 4 July 2022

Sanya avuta fomu kuwania tena Uenyekiti CCM Mkoa wa MaraMWENYEKITI wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara, Christopher Mwita Sanya (kushoto pichani juu), amechukua fomu ya kuwania tena nafasi hiyo.

Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Langael Akyoo amemkabidhi Sanya fomu hiyo ofisini kwake mjini Musoma leo, na mkutakia kila la heri katika kinyang’anyiro hicho.

Sanya ambaye aliwahi kutumikia nafasi hiyo mwaka 2012 hadi 2017, amekuwa mwanachama wa 10 kuchukua fomu ya kwania kiti hicho mwaka huu.

Sanya akijaza fomu ya kuwania nafasi hiyo

Katika utumishi wake, Sanya alipata umaarufu kutokana na kuhamasisha uhai wa CCM, ikiwemo kufungua matawi mengi, kufanikisha ukarabati wa ofisi ya CCM Mkoa iliyoko katani Nyasho na kusimamia kwa ufanisi utekelezaji wa ilani ya chama hicho tawala.

Sanya anakumbukwa pia kwa kusimamia uwajibikaji wa viongozi wa Serikali na utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyoainishwa kwenye ilani ya CCM, ikiwemo kuzielekeza halmashauri za mkoani Mara kuvipatia vikundi vya vijana, wanawake na wenye walemavu mikopo kwa wakati.

(Mwandishi: Maximillian Ngesi wa Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages