NEWS

Thursday 25 August 2022

Watumishi Tarime Mji wakumbushwa umakini kwenye uandaaji wa takwimu
Na Mara Online News
----------------------------

WATUMISHI wa Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, wamekumbushwa kuwa makini katika kuandaa na kutoa takwimu za vitu mbalimbali vinavyohusika kwenye shughuli za idara zao.

Msisitizo huo umetolewa na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Daniel Komote, katika kikao cha Baraza la Madiwani cha kupokea taarifa za kata, kilichofanyika kwenye ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Tarime, leo Agosti 25, 2022.

Komote ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Nkende, amehimiza suala hilo baada ya madiwani kulazimika kufanya marekebisho ya baadhi ya takwimu za taarifa za kata zilizowasilishwa kikaoni.

Kila diwani amewasilisha taarifa ya maendeleo ya kata yake katika halmashauri hiyo inayoundwa na kata nane.

Kutoka kushoto ni Makamu Mwenyekiti, Thobias Ghati, Mwenyekiti Daniel Komote, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Gimbana Ntavyo na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete, kikaoni leo.

Mwenyekiti huyo ametumia nafsi hiyo pia kutoa wito wa kuhamasisha wakazi wa halmashauri hiyo kuonesha ushirikiano wa dhati kwa makarani wa Sensa ya Watu na Makazi inayoendelea.

Baada ya madiwani kujadili taarifa za kata, Komote ameahirisha kikao hicho na kufungua kikao cha kawaida cha Baraza la Madiwani, kabla ya kingine cha kufunga mwaka wa fedha 2021/2022.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages