NEWS

Saturday, 15 October 2022

Mwenyekiti UVCCM Tarime kupatikana katika uchaguzi wa marudio kesho Jumapili


Lilian Wankyo Marwa

Na Mara Online News
-------------------------------

MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Tarime, anatarajiwa kupatikana katika uchaguzi wa marudio kesho Jumapili Oktoba 16, 2022, baada ya matokeo ya uchaguzi wa kwanza kufutwa siku chacha zilizopita.

Katika uchaguzi wa kwanza, mwanachama Mwita Machomba aliibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Tarime, kabla ya matokeo hayo kutupiliwa mbali.

Yugen Keraryo Keraryo

Taarifa zilizoifikia Mara Online News leo jioni, zinasema uchaguzi huo wa mrudio utafanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Ualimu Tarime (TTC), huku safari hii Machomba akiwa siyo mgombea tena wa nafasi hiyo.

Walioteuliwa kuchuana katika kinyang’anyiro hicho kesho kuanzia saa 3:00 asubuhi, ni Lilian Wankyo Marwa, Yugen Keraryo Keraryo na Godfrey Philemon Gotora.

Godfrey Philemon Gotora

Huo ni uchaguzi wa pili kurudiwa ndani ya CCM wilayani Tarime, baada ya ule wa Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake (UWT) Wilaya kufutwa na kurudiwa mara mbili.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages