NEWS

Thursday 6 October 2022

UCHAGUZI DURU YA TATU UWT CCM TARIME: Hatimye Neema amshinda kwa kura 6 aliyepata kura 2 duru ya kwanzaNa Mara Online News
-------------------------------

HATIMAYE Neema Charles (pichani juu) ametangazwa mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) CCM Wilaya ya Tarime, katika uchaguzi wa 'mbinde' wa marudio uliofanyika leo Oktoba 6, 2022.

Kwa mujibu wa Katibu wa UWT Wilaya ya Tarime, Mwanaidi Mbisha, Neema ameshinda baada ya kuvuna kura 184 dhidi ya mshindani wake, Scholastica Chacha aliyepata kura 178.

“Uchaguzi umeenda salama na kwa amani,” Mwanaidi ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu, muda mfupi baada ya uchaguzi huo kukamilika katika ukumbi wa TTC, nje kidogo ya mji wa Tarime.

Katika duru ya kwanza ya uchaguzi huo hivi karibuni, Neema alishinda kwa kupata kura 182 akifuatiwa na Joyce William aliyepata kura 180 na Scholastica (kura 2).

Hata hivyo, matokeo hayo yalifutwa na uchaguzi huo kurudiwa siku chache baadye, ambapo katika duru ya pili - Joyce aliyekuwa akitetea nafasi hiyo alitangazwa mshindi baada ya kupata kura 229 dhidi ya Neema (kura 138).

Hali kadhalika, matokeo ya uchaguzi huo wa duru wa pili nayo yalifutwa na CCM kwa madai ya ukiukwaji wa taratibu na kuelekeza urudiwe leo, huku safari hii Joyce akiwa ameenguliwa katika kinyang’anyiro hicho.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages