NEWS

Tuesday, 18 November 2025

Jaji Mkuu Mstaafu Chande kuongoza Tume Huru kuchunguza uvunjifu wa amani Uchaguzi Mkuu



Mohamed Chande Othman

Na Mwandishi Wetu

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji Mkuu Mstaafu Mohamed Chande Othman kuongoza Tume Huru itakayochunguza matukio ya uvunjifu wa amani yaliyotokea nchini wakati na baada ya Uchaguzi uliofanyika Oktoba 29, 2025.

Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Chamwino jijini Dodoma jana, iliwataja wajumbe wengine wa Tume hiyo kuwa ni Jaji Mkuu Mstaafu Prof. Ibrahim Hamis Juma, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Ombeni Yohana Sefue na Balozi Mstaafu Radhia Msuya.

Wengine ni Balozi Mstaafu Luteni Jenerali Paul Meela, Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu Said Mwema, Balozi Mstaafu David Kapya na Stergomena Lawrence Tax.

Rais Samia alieleza nia ya kuunda Tume hiyo hivi karibuni alipokuwa akifungua Bunge la 13 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages