Patrick Chandi Marwa
Na Sauti ya Mara, Musoma
---------------------------------------
KADA wa CCM na mfanyabiashara maarufu kutoka wilayani Serengeti, Patrick Chandi (pichani), ameibuka mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, katika uchaguzi uliotamalaki amani.
Katika uchaguzi huo uliofanyika mjini Musoma jana, Chandi alivuna kura 635 na kuwashinda wagombea wenzake; Joshua Mirumbe aliyepata kura 433 na Leonard Kitwara aliyeambulia kura 11.
Hivyo Msimamizi wa Uchaguzi huo, Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga alimtangaza Chandi kuwa Mwenyekiti mpya wa CCM Mkoa wa Mara kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.
Mwenyekiti aliyepita, Samwel Kiboye “Namba Tatu”, jina lake ‘lilikatwa’ kwenye vikao vya juu vya chama hicho tawala - alipoomba kuteuliwa kutetea nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment