NEWS

Sunday 27 November 2022

Naibu Waziri Silinde akagua ujenzi wa madarasa Tarime Vijijini, ataka kasi iendelee yakamilike kwa wakatiNa Mara Online News
-----------------------------------

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais - TAMISEMI (Elimu), David Silinde (wa pili kulia pichani juu), leo Novemba 27, 2022 amekagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) mkoani Mara na kutaka kasi aliyoikuta iendelee ili yakamilike kwa wakati.

“Ninatoa rai kasi hii iendelee, madarasa yote katika halmashauri hii yakamilike kwa wakati na mtoe taarifa mkoani ili nao watuletee, kwa sababu na sisi tuna lengo la kumkabidhi Rais madarasa yote 8,000 yakiwa yamekamilika,” Silinde alisema mara baada ya kukagua ujenzi wa madarasa mawili katika Shule ya Sekondari Nyantira.

Amesema yupo katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa maeneo mbalimbali nchini, kutokana na fedha zilizotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ili kuwezesha wanafunzi wote watakaochguliwa kuingia kidato cha kwanza mwaka 2023 wanapata nafasi.

“Rais ametoa fedha za madarasa 8,000 nchini ili watoto wote wapate nafasi kama alivyofanya mwaka jana [2021],” Naibu Waziri Silinde amesema na kuwataka viongozi husika kuhakikisha yanakamilika kwa wakati.

Awali, uongozi wa Shule ya Sekondari Nyantira umemueleza waziri huo kuwa wamepokea kutoka serikalini shilingi milioni 40 ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa - ikiwa ni maadalizi ya mapokezi wanafunzi kidato cha kwanza mwaka 2023.

“Ujenzi ulianza Oktoba 20, 2022 na utakamilika Desemba 10, 2022. Changamoto iliyopo ni kupnd kwa bei ya vifaa vya ujenzi, hasa saruji na mabati,” imeeleza sehemu ya taarifa ya ujenzi huo iliyotolewa na uongozi wa shule hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages