NEWS

Thursday, 29 December 2022

NGOs za Tarime zakutana na kuazimia kulishitaki gazeti la Sauti ya Mara



Na Mara Online News
------------------------------------

Viongozi na wajumbe wa Mashirika Yasiyokuwa ya Kiserikali (NGOs) yaliyopo wilaya ya Tarime mkoani Mara, yamekutana na kuazimia mambo sita ya kukabiliana na gazeti la Sauti ya Mara, likiwemo la kulishitaki.

Mkutano huo umekuja siku chache baada ya gazeti la Sauti ya Mara kuchapisha makala ya uchambuzi iliyoangazia mwendelezo wa vitendo vya ukeketaji licha ya kuwepo kwa NGOs nyingi zinazojipambanua kupiga vita mila hiyo.

Vyanzo vyetu vya habari vya uhakika vimesema mkutano huo umefanyika katika mojawapo ya hoteli za kifahari mjini Tarime, leo Desemba 29, 2022.

Viongozi na wajumbe wa mkutano huo kwa mujibu wa nakala ya mahudhurio ambayo Mara Online News imeiona, wametoka mashirika ya ATFGM Masanga, CDF, WAWETA, WWA, Care for Africa, Sachita, SHIWATA na Mkono wa Maendeleo Vijijini, miongoni mwa mengine.

Mwandishi wa habari pekee aliyealikwa na kuhudhuria mkutno huo ni mwakilishi wa RFA/Star Tv na CLEO 24 TV wa wilayani Tarime (jina lipo). Hata hivyo haijajulikana iwapo amealikwa kama mjumbe, au kwa ajili ya kuandika habari za mkutano huo.

Pamoja na mambo mengine, mkutano huo umeazimia gazeti la Sauti ya Mara lishitakiwe na libebe gharama zote za uendeshaji wa shitaka.

Bado haijajulikana mkutano huo umegharimiwa na shirika gani.

Hata hivyo Mara Online News na chombo dada chake, yaani gazeti la Sauti ya Mara havijapata rasmi malalamiko ya NGOs hizo kuhusiana na makala ya uchambuzi inayotajwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages