NEWS

Monday 23 January 2023

Mbunge Waitara awapa walimu, wazazi maelekezo kuinua ufaulu wa wanafunzi shule za sekondari Tarime VijijiniNa Mwandishi Wetu, Tarime
-------------------------------------------

MBUNGE wa Tarime Vijijini, Mwita Waitara (pichani juu kushoto), amewahimiza walimu na wazazi wa wanafunzi wa shule za sekondari jimboni humo kutekeleza majukumu yao ipasavyo ili kuinua kiwango cha ufaulu wa mitihani ya kitaifa.

Ametaja majukumu hayo kuwa ni pamoja na walimu kuongeza bidii ya kufundisha na wazazi kuhakikisha wanatoa chakula kwa ajili ya watoto wao wawapo shuleni.


Waitara ametoa maelekezo hayo mapema asubuhi leo Januari 23, 2023 alipofanya ziara katika Shule ya Sekondari Kemakorere kufuatilia matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Pili Mwaka 2022, ambayo hata hivyo ameeleza kutoridhishwa na kiwango cha ufaulu.

Mbunge huyo kutoka chama tawala - CCM na ambaye kitasnia ni mwalimu, ametumia nafasi hiyo pia kuelekeza wazazi kushirikiana na walimu kukomesha tatizo la utoro kwa wanafunzi - ambalo linatajawa kuchangia ufaulu usioridhisha kwenye shule hiyo, miongoni mwa nyingine katika jimbo la Tarime Vijijini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages