NEWS

Tuesday 24 January 2023

Rais Samia atengua uteuzi wa DC Mbarali, Wakurugenzi wanne akiwemo wa MusomaNa Mwandishi Wetu
-------------------------------

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassan (pichani), ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya (DC) mmoja na Wakurugenzi Watendaji wa Wilaya wanne.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jioni na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Zuhura Yunus, imewataja viongozi waliotenguliwa kuwa ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali, Reuben Ndiza Mfune.

Wakurugenzi waliotenguliwa na halmashuri za wilaya walizokuwa wakitumikia zikiwa kwenye mabano, ni Msongela Nitu Palela (Musoma mkoani Mara) na Michael Augustino Matomora (Iramba - Singida).

Wengine ni Linno Pius Mwageni (Ushetu - Shinyanga) na Sunday Deogratius Ndori (Ludewa - Njombe).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages