NEWS

Friday, 7 November 2025

Baraza la Habari Tanzania kukutanisha wadau kutafakari madhila yaliyotokea Uchaguzi Mkuu



Ernest Sungura

Na Mwandishi Wetu

Baraza la Habari Tanzania (MCT) litawakutanisha wadau wa habari nchini kujadili uhuru wa sekta hiyo kufuatia vurugu zilizojitokeza wakati wa Uchaguzi Mkuu wa Rais, Wabunge na Madiwani uliofanyika nchini Oktoba 29, 2025.

Taarifa iliyotolewa na MCT jijini Dar es Salaam jana Novemba 6, ilieleza kuwa madhila ya uchaguzi huo yameacha maswali mengi iwapo kila mdau alitekeleza wajibu wake kwa uaminifu na uadilifu - hatua ambayo iingeweza kuzuia maafa yaliyolikumba taifa.

Taarifa hiyo ambayo ilisainiwa na Katibu Mtendaji wa MCT, Ernest Sungura, imegusia masuala mbalimbali kama vile udhibiti wa intaneti ambao uliliweka taifa katika giza kujua matukio baada ya uchaguzi na ukweli halisi wa nini kilichokuwa kikitokea.

Taasisi zinazotarajiwa kukutana ni Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB), Ofisi ya Msemaji Mkuu wa Serikali, asasi na taasisi za habari zinazounda Umoja wa Haki ya Kupata Taarifa (CoRI).

Lengo la mkutano huo ni kutafakari kwa pamoja madhila ya Uchaguzi Mkuu huo na nafasi ya sekta ya habari katika kuleta upatanishi wa kitaifa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages