NEWS

Wednesday 4 January 2023

Rais wa Shirika la SACHITA azishangaa NGOs za Tarime, akana kushiriki kikao chao, azitaka zikubali kukosolewa na kujirekebisha



Na Mara Online News
------------------------------------

RAIS wa Shirika lisilo la Kiserikali la Save Children of Tanzania (SACHITA), Peter Mwera (pichani), amesema shirika lake halihusiki katika mgogoro unaotangazwa na baadhi ya Mashirika Yasio ya Kiseriklai (NGOs) wilayani Tarime, didhi ya vyombo vya habari vya Mara Online.

“Mimi nasema Mara Online na gazeti lao la Sauti ya Mara wanafanya kazi nzuri na tutaendelea kufanya nao kazi bega kwa bega,” amesema Mwera katika mazungumzo na Mara Online News kwa njia ya simu mapema asubuhi leo.

Aidha, Rais huyo wa SACHITA ambaye pia ni mmoja wawekezaji wazawa katika sekta za elimu, uvuvi, afya, habari na mwasiliano mkoani Mara, amesema shirika lake hilo halikuwa na mwakilishi kwenye kikao kilichofanyika hivi karibuni katika mojawapo ya hoteli za kifahari mjini Tarime na kuazimia kulishitaki gazeti la Sauti ya Mara.

Katika kikao hicho, viongozi na wajumbe wa baadhi ya NGOs zilizopo wilayani Tarime waliazimia kulishitaki gazeti la Sauti ya Mara, baada ya kuchapisha makala ya uchambuzi iliyooangazia kuendelea kwa tatizo la ukeketaji wilayani Tarime, licha ya kuwepo kwa NGOs nyingi zinazojipambua kupinga vita ukeketaji huku zikipata fedha kutoka wafadhili yakiwemo mashirika ya kimataifa.

Mara Online News imeona na nakala za maazimio ya kikao hicho na orodha ya mahudhurio inayoonesha kuwa SACHITA iliwakilishwa na mtu aliyejitambulisha kwa jina Paschal S Soko - akiwa wa tano kusaini kwenye fomu ya mahudhurio katika kikao hicho. Haijajulikana kikao hicho kilifadhiliwa na mtu, au na shirika gani.

“Mimi kama Rais wa SACHITA sijashiriki kikao hicho, hivyo hicho kikao sikitambui,” Mwera amesisitiza na kutaka asihusishwe na maazimio yaliyofikiwa na NGOs hizo.

Kwa upande mwingine, Mwera ameeleza kushangazwa na kitendo cha baadhi ya viongozi na wajumbe wa NGOs hizo kuhamaki na kutokubali kukosolewa katika jambo lililo wazi.

“Kukosolewa ni jambo zuri, kama wanakosolewa si wajirekebishe, kama wamefanya makosa wajirekibshe,” amesema Mwera ambaye shirika lake lilikuwa miongoni mwa mashirika ya kwanza kuendesha kampeni za kutoa elimu ya kupiga vita ukeketaji na ndoa za utoto wilayani Tarime katika miaka ya hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages