
Hussein Mohamed Bashe
Na Mwandishi Wetu
Aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Hussein Mohamed Bashe, ni mmoja wa mawaziri saba waliotupwa nje ya baraza jipya la mawaziri lililotangazwa na Rais Samia Suluhu Hassan.
Nafasi za mawaziri hao zimechukuliwa na wabunge wengine kufuatia Uchaguzi Mkuu uliofanyika nchini Oktoba 29, 2025.
Waziri mwingine aliyeachwa katika uteuzi wa Rais Samia alioutangazwa jana Ikulu, Chamwino jijini Dodoma, ni aliyekuwa Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko.
Mawaziri walioachwa ni Pindi Chana (Maliasili na Utalii), Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani), Stagomena Tax (Ulinzi na Jeshi ka Kujenga Taifa), Jenista Mhagama (Afya), Selemani Jafo (Viwanda na Biashara), Damas Ndumbaro (Katiba na Sheria) na Innocent Bashungwa (Mambo ya Ndani ya Nchi).
Mawaziri wapya waliochukua nafasi za walioachwa ni pamoja na Daniel Chongolo (Kilimo), Deogratias Ndejembi (Nishati), Rhimo Nyansaho (Ulinzi na Jeshi lka Kujenga Taifa), Mohamed Mchengerwa (Afya), Simbachawene (Mambo ya Ndani ya Nchi) na Juma Homera (Katiba na Sheria).
Baraza jipya mawaziri linaloapishwa leo Jumanne na Rais Samia linatarajiwa kuweka mikakati ya kuifikisha Tanzania kwenye uchumi wa juu wa kati kama ilivyo kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
No comments:
Post a Comment