Na Mara Online News
------------------------------------
WASICHANA 70 wameripotiwa kukeketwa siku chache baada ya kurudi nyumbani kwao wakitokea NGO ya ATFGM Masanga walikokuwa wamekimbilia na kuishi huko kwa mwezi mzima kukwepa ukeketaji.
Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee (pichani katikati), amefika kituoni hapo leo na kuliagiza Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya kuwakamata wazazi wa wasichana hao kwa hatua za kisheria.
Haijajulikana sababu hasa ya wasichana hao kukeketwa - licha ya kuishi katika NGO ya ATFGM Masanga inayojipambanua kutoa elimu ya kupiga vita ukeketaji.
Mara Online news itaendelea kukuhabarisha zaidi juu ya suala hilo kadiri inavyopata taarifa husika, zikiwemo za utekelezaji wa agizo lililotolewa na Mkuu wa Mkoa.
No comments:
Post a Comment