NEWS

Tuesday 10 January 2023

RC Mara aahidi msaada Nyumba Salama Mugumu inayoendeshwa na Shirika la Hope for Girls



Na Mara Online News
-----------------------------------

MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee (pichani katikati), ametembelea kituo cha Nyumba Salama Mugumu wilayani Serengeti leo na kupongeza kazi nzuri inayofanywa na Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania linalokiendesha.

Kituo hicho ni maalumu kwa ajili ya kuwahifadhi na kuwapa huduma za msingi watoto wa kike wanaokimbia ukeketaji, ukatili na unyanyasaji mwingine wa kijinsia.

RC Mzee ameahidi kutoa shilingi milioni mbili kuchangia uendeshaji wa kituo hicho chini Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania ambalo Mkurugenzi wake ni Rhobi Samwelly (wa pili kulia pichani).

Aidha, kiongozi huyo wa mkoa ametumia nafasi hiyo pia kutoa wito kwa watu kuachana na mila ya ukeketaji, la sivyo mamlaka za Serikali hizitasita kuwakamata na kuwachukulia hatua kali za kisheria.

Hadi sasa Shirika la Hope for Girls and Women Tanzania linaloendesha vituo vya Nyumba Salama Mugumu na Butiama mkoani Mara, limeshafanikiwa kuokoa wasichana zaidi ya 4,000 waliokuwa katika hatari ya kukeketwa na kufanyiwa ukatili mwingine wa kijinsia.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages