NEWS

Thursday, 2 February 2023

Mwili wa aliyewahi kuwa RC Mara, Balozi Nimrod Lugoe kuzikwa leo


Balozi Nimrod Lugoe enzi za uhai

Na Mwandishi Wetu
--------------------------------

MWILI wa Balozi Nimrod Lugoe unatarajiwa kuzikwa leo Alhamisi Februari 2, 2023 katika makaburi ya Kondo, maeneo ya Bahari Beach/Ununio, jijini Dar es Salaam.

Balozi Lugoe ambaye ni mzaliwa wa kijiji cha Suguti katika jimbo la Musoma Vijijini mkoa wa Mara, alifariki dunia usiku wa kuamkia Januari 30, 2023.

Balozi Lugoe aliwahi kufanya kazi mbalimbali serikalini zikiwemo za Balozi wa Tanzania katika nchi za Uganda, Zimbabwe na Zambia kwa nyakati tofauti, kabla ya kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

“Heshima ya Tanzania kwenye ukombozi wa nchi za Kusini mwa Afrika, kwa kiasi kikubwa ilitokana na kazi ya akina Lugoe, Joshua Opanga na wengine kama wasaidizi, wakiwa Wizara ya Mambo ya Nje, kituo cha New York nchini Marekani, wakimsaidia Balozi Salim Ahmed Salim,” amesema aliyewahi kuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Kwanza wa Rais, Jaji Joseph Sinde Warioba, wakati akitoa salaamu za rambirambi katika msiba huo wa marehemu Balozi Lugoe.

Jaji Warioba na Balozi Lugoe walisoma pamoja katika Shule ya Sekondari ya Wavulana Bwiru, walipata kufanya kazi pamoja Wizara ya Mambo ya Nje na Ikulu na walikuwa marafiki wa karibu sana kwa muda wote.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages