NEWS

Friday 31 March 2023

Polisi aliyeua mwendesha bodaboda kwa risasi Tarime mbaroni


RPC Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya.

Na Mara Online News
------------------------------------

JESHI la Polisi linamshikilia askari wake mwenye utambulisho wa H 4489 PC Kululetela, kutokana na kosa la kumfyatulia risasi iliyomjeruhi hadi kumsababishia mauti mwendesha bodaboda, Ng'ondi Marwa (22), mkazi wa mjini Tarime.

Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Polisi Tarime Rorya, ACP Geofrey Sarakikya amewambia waandishi wa habari ofisini kwake leo jioni kuwa askari huyo kutoka Kituo cha Polisi Sirari anashikiliwa katika Kituo cha Polisi Tarime na kwamba upelelezi wa kesi yake utakamilika mapema kwa hatua zaidi za kisheria.

Kwa mujibu wa RPC Sarakikya, Marwa amepigwa risasi kwenye paja la kulia akiwa katika kitongoji cha Nyansisine kijijini Kubiterere leo Ijumaa Machi 31, 2023 saa mbili asubuhi.

Ameongeza kuwa kijana huyo amefariki dunia muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime na kwamba mwili wake umehifadhiwa hospitalini hapo kusubiri uchunguzi zaidi na taratibu za mazishi.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages