NEWS

Tuesday 28 March 2023

Uwekaji vigingi mpaka wa Hifadhi ya Serengeti na vijiji vinavyopakana nayo Tarime waingia siku ya piliNa Mara Online News
---------------------------------

KAZI ya uwekaji wa vigingi vya mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji vinavyopakana nayo upande wa wilaya ya Tarime mkoani Mara imeingia siku ya pili.

Taarifa zilizotufikia kutoka eneo la tukio mapema leo Machi 28, 2023 zinasema uwekaji vivingi umeendelea kijijini Kegonga, na kwamba baadhi ya wananchi waliopata ajira ya muda mfupi katika shughuli hiyo ni wakazi wa maeneo hayo.

"Hali ni shwari, kazi inendelea kwa amani na baadhi ya wanavijiji wamepata ajira," mkazi wa kijiji cha Kegonga aliyejitambulisha kwa jina la Marwa ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu.

Akizindua uwekaji wa vigingi vya mpaka huo kijijini Kegonga jana, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee alitoa onyo kwa viongozi wa kisiasa wanaojaribu kuchonganisha wananchi na serikali ili kukwamisha shughuli hiyo. “Nawaonya… msijione mko juu ya sheria,” alisisitiza.

Uwekaji wa vigingi hivyo ni utekelezaji wa maamuzi ya Baraza la Mawaziri kutokana na ushauri wa Kamati ya Mawaziri Wanane wa Kisekta iliyoundwa na Serikali ya Awamu ya Tano kukusanya maoni ya ufumbuzi wa migogoro ya ardhi kati ya wananchi na Hifadhi za Taifa nchini, ikiwemo Serengeti.

#Tuhakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages