NEWS

Wednesday 29 March 2023

TANAPA yawezesha wanavijiji Tarime ziara ya kujifunza faida za uwekezaji na uhifadhi


Baadhi ya wananchi na viongozi  kutoka vijiji vya kata za Nyanungu na Kwihancha wilayani Tarime wakiwa katika Hoteli ya Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa Serengeti wakati wa ziara yao ya mafunzo.


Na Mara Online News
------------------------------------

SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limewezesha baadhi ya viongozi na wananchi (pichani) kutoka vijiji vinavyopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara, kufanya ziara ya mafunzo ya kupata uelewa kuhusu faida za uwekezaji wa hoteli za kitalii na uhifadhi endelevu.

Viongozi na wananchi hao wakiwemo wa vijiji vya Kegonga na Nyandage vilivyopo kata ya Nyanungu na vijiji vya kata ya Kwihancha, walifanya ziara hiyo hivi karibuni katika Hifadhi za Taifa za Serengeti, Manyara, Ngorongoro na Jumuiya ya Uhifadhi wa Wanyamapori ya IKONA.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Izumbe Msindai, ziara hiyo ililenga kuwawezesha kujionea jinsi wananchi wa maeneo mengine wanavyonufaika kiuchumi na kijamii baada ya kukaribisha wawekezaji wa hoteli za kitalii katika maeneo yao yanayopakana na hifadhi.
Mhifadhi Izumbe Msindai

“Tuliwawezesha kutembelea na kujifunza kwa wengine ili waweze kubadilisha fikra na uelewa juu ya uhifadhi na jinsi wanavyoweza kutumia fursa ya maeneo yao yanayopakana na hifadhi kunufaika kiuchumi. Maeneo yao ni mazuri sana kwa uwekezaji na tunatumaini yatawanyanyua zaidi kiuchumi kuliko jinsi walivyo sasa,” alisema Msindai.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages