NEWS

Wednesday 12 April 2023

Bikoni yaripotiwa kung'olewa mpaka wa Nyanungu na Hifadhi ya Serengeti

 



Na Mara Online News

Mojawapo ya bikoni ambazo zimewekwa kwenye mpaka wa Hifadhi ya Taifa Serengeti na  kijiji cha Kegonga - kata ya Nyanungu wilayani Tarime imeripotiwa kuvunjwa na kung’olewa na watu wasiojulikana .

Taarifa za hivi punde ambazo zimefikia Mara Online News zinasema bikoni hiyo iling’olewa  katika kitongoji cha Giyema , kijiji cha Kegonga usiku wa kuamkia jana Aprili 11, 2023.

Viongozi wa vijiji na vitongojii katika eneo hilo wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo bila kutoa taarifa zaidi.
Hata hivyo Mara Online News imepata taarifa kuwa maafisa  wa jeshi la polisi tayari wamezuru kijijini Kegonga kufanya uchunguzi wa tukio hilo.
Baadhi ya wananchi wamelaani waliohusika kufanya tukio hilo.

“ Hawa wanaoharibu bikoni wanakosea  kwa sababu malalamiko yetu yapo ofisini – serikalini “, amesema mwananchi mmoja wa kijijinji Kegonga kwa njia ya simu.


Serikali inatekeleza mpango wa kuweka bikoni hizo ili kutatua mgogoro wa muda mrefu wa kugombea mpaka wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na vijiji vinavyokana nayo upande wa wilaya ya Tarime, vikiwemo Kegonga na Nyandage vya katani Nyanungu.

Kazi ya kuweka bikoni hizo katika vijiji viwili vya vya Kegonga na Nyandage vya kata ya Nyanungu ilikamilika siku chache zilizopita huku kazi hiyo ikiripotiwa kuendelea kwa amani katika kata jirani za Gorong’a na Kwihancha .


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages