NEWS

Tuesday 11 April 2023

Makamu wa Rais kufungua kikao kazi cha watendaji wa Mahakama ya Tanzania jijini Mwanza kesho


Makamu wa Rais, Dkt Philip Mpango.

Na Pius Rugonzibwa, Mwanza
---------------------------------------------

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango anatarajiwa kufungua kikao kazi cha watendaji wa Mahakama ya Tanzania kitakachofanyika jijini Mwanza kesho.

Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi za Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza leo, Msajili Mkuu wa Mahakama, Wilbert Chuma amesema kikao kazi hicho kitajadili masuala kadhaa, ikiwa ni pamoja na taarifa za utendaji wa Mahakama kwa mwaka 2022 na mkakati wa maboresho ya chombo hicho cha kisheria.

Mada nyingine amesema zitahusu mwongozo wa ukaguzi wa shughuli za kimahakama, mfumo wa usimamizi wa mashauri na tathmini ya kina juu ya shughuli za mahakama na maboresho yake kwa manufaa ya umma.
Kutoka kulia ni Msajili Mkuu wa Mahakama, Wilbert Chuma, Mtendaji Mkuu wa Mahakama, Prof Elisante Ole Gabriel na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania, Dkt Anjelo Rumisha - wakati wa mkutano na waandishi wa habari jijini Mwanza leo.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages