NEWS

Tuesday 2 May 2023

Bibi na wajukuu waliopoteza maisha kwa kusombwa na maji Tarime kuzikwa keshoNa Mara Online News
-----------------------------------

MIILI ya watu watatu wa familia moja waliokufa kwa kusombwa na maji katika mtaa wa Bomani wilayani Tarime, Mara itazikwa kesho Jumatano, viongozi wa mitaa husika wamethibitisha.

“Kwanza msiba umehamishiwa kwa ndugu wa maheremu katika mtaa wa Iganana kwa sababu nyumba yao ilisombwa na maji. Kesho maziko yatafanyika katika makaburi ya Magena,” Mwenyekii wa Mtaa huo, John Omahe ameiambia Mara Online News mapema leo asubuhu.

Omahe na viongozi wa mtaa wa Bomni wameishukuru Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Tarime chini ya Mkuu wa Wilaya hiyo, Kanali Michael Mntenjele kutoa msaada wa kufanikisha shughuli za mazishi hayo.

Waliopoteza maisha kwa kusombwa na maji ni Ghati Amon Mwita (69) na wajukuu wake; Vilet Denis (3) na Johnson Denis (10).

Watu hao walifariki dunia baada ya nyumba yao (pichani chini) kusombwa na maji juzi wakati wa mvua kubwa iliponyesha na kusababisha mafuriko mto ulio jirani na nyuma hiyo.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages