NEWS

Monday 15 May 2023

Mgodi wa Barrick North Mara wakarabati tena barabara ya Uwanja wa Ndege - NyamwagaNa Mara Online News
-----------------------------------

MGODI wa Dhahabu wa North Mara uliopo Nyamongo wilayani Tarime, umeendeleza utaratibu wake wa kukarabati barabara za changarawe katika vijiji vinavyopakana nao ili kurahisishia wananchi usafiri.

Jana, Mara Online News ilishuhudia katapila la Kampuni ya Barrick likikarabati tena barabara ya Uwanja wa Ndege - Nyamwaga iliyokuwa imeanza kuharibika kutokana na mvua zilizonyesha, ikiwa ni miezi miwili imepita tangu liikarabati.
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania, kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages