NEWS

Saturday, 13 December 2025

Mtanzania Bhoke Nyambari Nyangwine avunja rekodi ya ufaulu Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza



Bhoke Nyambari Nyangwine (katikati mbele) akiwa mwenye furaha baada ya kupokea Shahada ya Uzamili ya Sheria (LLM) katika Chuo Kikuu cha Manchester, Uingereza.

Na Mwandishi Wetu

Kwa mara nyingine tena, Mtanzania Bhoke Nyambari Nyangwine, ameibuka na ufaulu wa kishindo wa daraja la juu (distinction) katika Shahada ya Uzamili ya Sheria (LLM) katika Chuo Kikuu cha Manchester nchini Uingereza, wiki hii.

Bhoke (22), ambaye ni binti wa mfanyabiashara, mwandishi na mchapaji wa vitabu maarufu Tanzania, Nyambari Nyangwine, ambaye amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime mkoani Mara, mwaka 2010 hadi 2015.


Bhoke Nyambari Nyangwine akiendelea na furaha ya ufaulu huo

Bhoke alimaliza masomo ya miaka mitatu ya Shahada yake ya Kwanza ya Sheria (LLB) katika chuo hicho, mwaka jana na kupata ufaulu wa daraja la kwanza (First Class, with hons).


Bhoke Nyambari Nyangwine akitabasamu kwa ufaulu huo

Akizungumza na Mara Online News kwa njia ya simu jana baada ya kupokea shahada yake, Bhoke alisema matokeo hayo mazuri yanatokana na bidii yake katika masomo, kuwezeshwa na wazazi wake na kumtanguliza Mungu kwa kila kitu.

“Namshukuru Mungu kwa matokeo haya. Wazazi wangu walinitia moyo na mimi sikuwaangusha,’’ alisema Bhoke huku akitabasamu.


Bhoke Nyambari Nyangwine akifurahia picha ya pamoja na mmoja wa walimu (lecturers) wa Chuo Kikuu cha Manchester

Bhoke anaona fahari kuwa msomi mwenye Shahada ya Uzamili ya Sheria (LLM) kutoka Chuo Kikuu maarufu cha Manchester, nchini Uingereza.

Alitoa wito kwa wazazi, walezi na jamii kwa ujumla kuwezesha watoto wa kike kufikia ndoto zo kielimu kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.

Bhoke Nyambari Nyangwine akifurahia picha ya pamoja na mmoja wa wakuu (deans) wa Chuo Kikuu cha Manchester

Bhoke ambaye ni mtoto wa kwanza wa Nyambari Nyangwine, alipata elimu ya msingi na sekondari, kidato cha kwanza hadi cha sita katika Shule ya Dar es Salaam Independent School (DIS), kabla ya kujiunga na Chuo Kikuu Cha Manchester, nchini Uingereza.


Bhoke Nyambari Nyangwine akifurahia picha ya pamoja na mmoja wa rafiki zake chuoni hapo

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages