NEWS

Monday 29 May 2023

RC Mtanda aahidi msako mkali walioua watu wanne Butiama

RC Mtanda (katikati) akishiriki mazishi ya mmoja wa watu wanne waliouawa wilayani Butiama

Na Mara Online News
--------------------------------

MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Said Mohamed Mtanda amekemea vikali mauaji ya watu wanne yaliyotokea wilayani Butiama, na kuahidi kushirikiana na wananchi kutokomeza vitendo hivyo.

RC Mtanda ameyasema hayo leo Jumatatu Mei 29, 2023 wakati akizungumza na waombolezaji katika kitongoji cha Kuoko kilichopo kijiji cha Nyamikoma, Butiama alipokwenda kutoa salamu za pole katika msiba wa marehemu Mwandu Malegesi, mmoja wa hao waliouawa na watu ambao hawajajulikana usiku wa Mei 27, 2023 kijijini hapo.

Amewaomba wananchi kuwa watulivu kipindi hiki wakati Jeshi la Polisi likiendelea kuwatafuta wote waliohusika katika mauaji hayo.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages