Na Mwandishi Wetu, Mvomero
----------------------------------------------
TAASISI ya Tete Foundation imeungana na jamii kuadhimisha Siku ya Hedhi Duniani, ambapo imetumia nafasi hiyo kutangaza Kampeni yake ya mwaka huu ya Sitakosa Shule.
Akizungumza wakati wa maadhimisho hayo yaliyofanyika katika kituo na Shule Amani iliyopo wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro jana Mei 28, 2023, Mkurungezi wa Taasisi hiyo, Suzana Senso alisema takwimu zinaonesha kuwa mtoto wa kike hukosa darasani siku tano hadi saba kutokana na kushindwa kujisitiri anapokuwa kwenye hedhi.
“Mwaka huu Taasisi yetu imekuja na dhima ya “Sitakosa Shule Campaign” ambapo mwaka huu tunagawa taulo za kike za kutumia kwa muda wa miezi sita kwa mabinti zaidi ya 50 waliopo kwenye shule ya Amani,” alisema Suzana.
Aidha, Mkurugenzi Suzana huyo aliwashukuru wadau walioshirikiana na Tete Foundation kufanikisha shughuli hizo, ikiwemo UAP Insurance Tanzania.
Bila kusahau wazalishaji wa taulo za kike za HQ PAD na Love of Christ Ministry kwa kuwa sehemu ya kuhakikisha kila mtoto wa kike wa Shule ya Amani hakosi darasani kwa muda wa miezi sita kutokana na kuwa kwenye hedhi.
“Asante kwa kuwa sehemu ya kurudisha tabasamu kwa mtoto wa kike,” alisisitiza Mkurugenzi Suzana.
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi
No comments:
Post a Comment