NEWS

Saturday 6 May 2023

Mawaziri watua Tarime Vijijini kuwasikiliza wananchi wanaopakana na Hifadhi ya Serengeti




Na Mara Online News
-----------------------------------

MAWAZIRI watatu wa kisekta tayari wapo ndani ya wilaya ya Tarime mkoani Mara kutekeleza agizo la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa la kukutana na kuwasikiliza wananchi wanaopakana na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Mawaziri hao ni Angellah Kairuki wa Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Dkt Angeline Mabula (Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi) na Naibu Waziri Maliasili na Utalii, Mary Masanja.

Wamepokewa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Meja Jenerali Suleiman Mzee na Mbunge wa Tarime Vijijini, Mwita Witara kwa ajili ya kusikiliza hoja na mahitaji ya wananchi wa maeneo yanayopakana na Hifadhi ya Serengeti ili Serikali ivifanyie kazi.

Taarifa zilizotufikia hivi punde zinasema tayari mawaziri hao wamefanya mikutano na wananchi katika kata za Nyanungu  na Kwihancha .

Mikutano ya mawaziri hao inalenga kupata ufumbuzi wa kudumu wa mgogoro wa kugombea mpaka wa maeneo hayo na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages