NEWS

Tuesday, 4 July 2023

Serengeti wakabidhi Mwenge wa Uhuru wilayani Butiama



Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dkt Vincent Mashinji (kushoto) akikabidhi Mwenye wa Uhuru kwa Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mwl Moses Kaegele (katikati) mapema leo asubuhi.

Na Godfrey Marwa, Serengeti

----------------------------------------

MWENGE wa Uhuru umeingia wilayani Butiama mapema leo asubuhi baada ya kuhitimisha mbio zake katika wilaya ya Serengeti jana.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dkt Vincent Mashinji amekabidhi Mwenge huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Butiama, Mwl Moses Kaegele.

Ukiwa wilayani Serengeti, Mwenge wa Uhuru ulizindua miradi miwili, kuweka mawe ya msingi katika miradi mitatu na kutembelea kikundi cha vijana cha ufugaji wa kondoo katika kata ya Natta.



Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdallah Shaibu Kaim alieleza kuridhishwa na kazi nzuri iliyofanywa katika kusimamia na kutekeleza miradi ya maendeleo wilayani Serengeti.

Mfano akiweka jiwe la msingi katika miradi ya maji na zahanti katika kata ya Issenye, Shaibu alisema utekelezaji wa miradi hiyo unaakisi thamani ya fedha baada ya kupitia nyaraka zote husika.



Kiongozi wa huyo wa Mwenge wa Uhuru aliagiza wananchi ambao walitoa maeneo yao kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa maji katani Issenye kuwa wa kwanza kusambaziwa huduma ya maji ya bomba.

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages