NEWS

Wednesday 5 July 2023

Kiongozi Mwenge wa Uhuru akagua miradi ya elimu, afya, barabara Butiama




Na Godfrey Marwa, Butiama
-------------------------------------

KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2023, Abdalla Shaib Kaim leo Julai 5, 2023 amekagua na kuweka jiwe la msingi mradi wa ujenzi wa nyumba nne kila moja ikiwa pacha (two in one) za walimu katika Shule ya Sekondari ya Adam K Malima iliyopo kata ya Siroli-Simba wilayani Butiama, Mara.

Ujenzi wa mradi huo utagharimu shilingi milioni 230, kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kwa kiongozi huyo wa mbio za Mwenge wa Uhuru.

Awali, Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Shaim, aliweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara ya udongo katika kata ya Siroli-Simba yenye urefu wa kilomita 9.2 wenye thamani ya shilingi zaidi ya milioni 150.



Pia Kiongozi wa Mbio za Mwenge alitembelea, kukagua na kuzindua mradi wa Kituo cha Afya Butuguri wenye thamani ya shilingi milioni 537, kati ya hizo, shilingi milioni zilitolewa na Serikali Kuu na shilingi milioni 37 zilitolewa na Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.


Mwenge wa Uhuru unaendelea kukagua na kuzindua miradi ya maendeleo wilayani Butiama ikiwa ni baada ya kuhitimisha mbio zake wilayani Serengeti jana.

Mbio za Mwenge wa Uhuru zinatarajiwa kuingia katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini) kesho Alhamisi. 

#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages