Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele.
----------------------------
MKUU wa Wilaya (DC) ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele ametoa wito kwa wakazi wa eneo la Nyeheto kuchangamkia malipo yao ya fidia, ili kupisha upanuzi wa shughuli za Mgodi wa Dhahabu wa North Mara.
“Wachangamkie malipo yao ya fidia ili waweze kuondoka haraka iwezekanavyo kupisha uwekezaji wa mgodi huo,” DC Mntenjele amesisitiza katika mazungumzo na Mara Online News ofisini kwake leo.
Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hatua hiyo ya malipo ya fidia kwa wananchi hao imekuja baada ya mgogoro uliokuwepo katika eneo la Nyeheto kupata suluhisho.
Taarifa zilizopo zinaeleza kuwa Kampuni ya Barrick imetenga shilingi zaidi ya bilioni tano kwa ajili ya malipo ya fidia kwa wananchi wanaohamishwa kutoka eneo hilo ili kupisha upanuzi wa shughuli za mgodi wa North Mara.
Mgodi wa Dhahabu wa North Mara unaendeshwa na Kampuni ya Barrick kwa ubia na Serikali ya Tanzania kupitia Kampuni ya Twiga Minerals.
No comments:
Post a Comment