NEWS

Monday 11 September 2023

Waziri Gwajima awanyooshea kidole wazazi na walezi wanaotumia watoto kwenye ‘show’ za sherehe usikuWaziri Dorothy Gwajima

Na Mwandishi Wetu
--------------------------- 

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt Dorothy Gwajima ametoa onyo kali kwa wazazi, walezi na wote wanaotumia watoto kutumbuiza “show” kwenye sherehe zikiwemo harusi nyakati za usiku. 

“Nimeona video fupi ikisambaa na kuonesha watoto wakitoa SHOW usiku kwenye sherehe hivi kwa wimbo wenye miondoko isiyo ya afya kwa rika la watoto. 

“Ni kosa kisheria kutumia watoto kwenye matumizi ya aina hii kwa mujibu wa Sheria ya Mtoto Na. 21 ya Mwaka 2009 iliyorekebishwa mwaka 2019,” Waziri Gwajima aliandika kwenye ukurasa wake wa Istagram wiki iliyopita. 

Alisema ofisi yake itachukua hatua za kuwapata waliowatumia watoto kwenye sherehe hiyo ya usiku ili kuwaelimisha madhara yake na kuwaonya kutorudia kosa hilo. 

“Hata hivyo, wakati tukiandaa PRESS [akimaanisha mkutano na waandishi wa habari] wiki ijayo (wiki hii), natanguliza salaam hapahapa kuwa, jamii yote KUWENI MAKINI na SHERIA YA MTOTO. Iko humu mtandaoni SOMENI, vinginevyo tusilaumiane kwa hatua stahiki za kisheria,” Waziri Gwajima alielekeza katika taarifa yake hiyo. 

Chanzo: SAUTI YA MARA
#Tunakuhabarisha Ukweli kwa Weledi

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages