NEWS

Friday 27 October 2023

Spika Tulia Ackson ashinda Urais wa Umoja wa Mabunge Duniani

Dkt Tulia Ackson

SPIKA wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Tulia Ackson, amechaguliwa kuwa Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU) katika uchaguzi uliofanyika leo Oktoba 27, 2023 jijini Luanda, Angola wakati wa Mkutano wa 147 wa Umoja huo.

Dkt Tulia ameshinda uchaguzi huo mara baada ya kupata kura 172 sawa na asilimia 57 ya kura 303 zilizopigwa na wajumbe walioshiriki mkutano huo. 

Amewashinda wagombea wengine watatu ambao ni Adji Diarra kutoka Bunge la Senegal aliyepata kura 59, Catherine Hara Spika wa Bunge la Malawi (kura 61) na Marwa Hagi kutoka Bunge la Somalia (kura 11). 

Spika Tulia anakuwa Rais wa 31 wa IPU na pia mwanamke wa kwanza kutoka Bara la Afrika kushika wadhifa huo. 

Mara baada ya kuchaguliwa Dkt Tulia amewashukuru wajumbe wote kwa imani kubwa waliyoionesha kwake na kuahidi kutimiza yote alioahidi wakati wa kampeni.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages