NEWS

Wednesday 29 November 2023

Basi la Ally’s laparamia treni wilayani Manyoni, watu 13 wapoteza maisha, 25 wajeruhiwa
Na Mwandishi Wetu, Manyoni
-----------------------------------------


Watu 13 wamepoteza maisha na wengine 25 kujeruhiwa kutokana na ajali ya basi la Kampuni ya Ally’s lililoparamia kichwa cha treni wilayani Manyoni, Singida.

Ajali hiyo (pichani juu) imetokea leo Jumatano saa 10 alfajiri kwenye kivuko cha reli, baada ya basi hilo lenye namba za usajili T 178 DVB lililokuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza kugonga kichwa cha treni.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Stellah Mutabihiriwa, basi hilo lilikuwa limebeba abiria 57 na limegonga kichwa cha treni chenye namba za usajili V1951-9006 kilichokuwa kikitoka Itigi kuelekea Manyoni.

Mganga Mkuu wa Wilaya ya Manyoni, Dkt Furaha Mwakafwila amesema watu tisa wamefariki dunia kwenye eneo la ajali na wanne wakati wakipatiwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya na ile ya Mtakatifu Gasper iliyopo Itigi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Peter Serukamba ametembelea eneo la ajali hiyo, akiwa amefuatana na viongozi wengine wa vyombo vya ulinzi na usalama.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages