Mbunge Mwita Waitara akizungumza |
Na Mwandishi Wetu, Musoma
Mara Online News
------------------------------
Mara Online News
------------------------------
MBUNGE wa Jimbo la Tarime Vijijini, Mwita Waitara amewataka wananchi kuwapuuza viongozi na wanachama wa vyama vya upinzani wanaowachochea kutochangia shughuli za maendeleo katika maeneo yao.
Waitara ambaye anayetokana na chama tawala - CCM, alitoa kauli hiyo jana katika kata ya Bukima iliyopo jimbo la Musoma Vijijini, wakati wa ziara ya kimkoa ya Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Patrick Chandi.
“Nchi hii hapa tulipo ni pazuri, wapuzeni hao wanaotwambia mambo ya Ulaya. Unaambiwa usichangie shughuli za maendeleo, wanataka mkwame. Mkishikamana maendeleo yataenda kwa haraka,” alisema Waitara.
Alisema kata nyingi mkoani Mara zimepata maendeleo kwa sababu madiwani na wabunge wanatokana na CCM.
“Wapinzani ninawajua nje na ndani, wanachofanya wanachemsha mawe, ni ndege wasiofugika, kunguru asiyepikwa, akipikwa haivi, akiiva hanyweki supu wala kuliwa. Adui yako hawezi kukuchagulia rafiki, hata kwenye bandari tungewasikiliza tungekwama,” alisema.
Katika ziara hiyo, Mwenyekiti wa CCM Mkoa, Chandi, alitoa maelekezo ya kushughulikia utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi katika jimbo la Musoma Vijijini.
Mwenyekiti Chandi akizungumza katika kikao cha ndani Musoma Vijijini jana.
Leo Jumatatu, kiongozi huyo ambaye anaambatana na wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Mara anaendelea na ziara hiyo Musoma Mjini kuimarisha chama hicho na maendeleo.
No comments:
Post a Comment